Ephesians 6

Mafundisho Kuhusu Watoto Na Wazazi

1 aEnyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, kwa kuwa hili ni jema. 2 b“Waheshimu baba yako na mama yako,” hii ndio amri ya kwanza yenye ahadi, 3 c“upate baraka na uishi siku nyingi duniani.”

4 dNinyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu, bali waleeni kwa nidhamu na mafundisho ya Bwana.

Mafundisho Kuhusu Watumwa Na Mabwana

5 eNinyi watumwa, watiini hao walio mabwana zenu hapa duniani kwa heshima na kwa kutetemeka na kwa moyo mmoja, kama vile mnavyomtii Al-Masihi. 6 fWatiini, si tu wakati wakiwaona ili mpate upendeleo wao, bali mtumike kama watumwa wa Al-Masihi, mkifanya mapenzi ya Mungu kwa moyo. 7 gTumikeni kwa moyo wote, kama vile mnamtumikia Bwana na si wanadamu. 8 hMkijua kwamba Bwana atampa kila mtu thawabu kwa lolote jema alilotenda, kama yeye ni mtumwa au ni mtu huru.

9 iNanyi mabwana, watendeeni watumwa wenu kwa jinsi iyo hiyo. Msiwatishe, kwa kuwa mnajua ya kwamba yeye aliye Bwana wenu na Bwana wao yuko mbinguni, naye hana upendeleo.

Silaha Za Mungu

10 jHatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. 11 kVaeni silaha zote za Mungu ili kwamba mweze kuzipinga hila za ibilisi. 12 lKwa maana kushindana kwetu si juu ya nyama na damu, bali dhidi ya falme, mamlaka, dhidi ya wakuu wa giza na majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. 13 mKwa hiyo vaeni silaha zote za Mungu ili mweze kushindana siku ya uovu itakapokuja nanyi mkiisha kufanya yote, simameni imara. 14 nKwa hiyo simameni imara mkiwa mmejifunga kweli kiunoni na kuvaa dirii ya haki kifuani, 15 onayo miguu yenu ifungiwe utayari tuupatao kwa Injili ya amani. 16 pZaidi ya haya yote, twaeni ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu. 17 qVaeni chapeo ya wokovu na mchukue upanga wa Roho, ambao ni Neno la Mungu. 18 rMkiomba kwa Roho siku zote katika sala zote na maombi, mkikesha kila wakati mkiwaombea watakatifu wote.

19 sNiombeeni na mimi pia, ili kila nifunguapo kinywa changu, nipewe maneno ya kusema, niweze kutangaza siri ya Injili kwa ujasiri, 20 tambayo mimi ni balozi wake katika vifungo. Ombeni ili nipate kuhubiri kwa ujasiri kama inipasavyo.

Salamu Za Mwisho

21 uTikiko, aliye ndugu mpendwa na mtumishi mwaminifu katika Bwana, atawaambia kila kitu, ili pia mpate kujua hali yangu na kile ninachofanya sasa. 22 vNinamtuma kwenu kwa ajili ya kusudi hili hasa, ili mpate kujua hali yetu, na awatie moyo.

23 wAmani iwe kwa ndugu, na pendo pamoja na imani kutoka kwa Mungu Baba na Bwana Isa Al-Masihi. 24 xNeema iwe na wote wampendao Bwana wetu Isa Al-Masihi kwa upendo wa dhati. Amen.
Copyright information for SwhKC